Utawala wa Kizayuni wa Israel umetangaza kwamba utakata uhusiano
wake na Mamlaka ya Ndani ya Palestina, baada ya kuundwa serikali ya
umoja wa kitaifa ya Palestina. Kiongozi mmoja wa utawala huo ghasibu
ameiambia ofisi ya Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina kwamba, utawala
wa Kizayuni utakata mahusiano yote na mamlaka hiyo, isipokuwa katika
masuala ya kiusalama.
Hapo jana, viongozi wa Israel walitangaza kwamba, kamwe hawatatoa
fursa kwa mawaziri watatu wa serikali ya umoja wa kitaifa kutoka Ghaza
kuelekea Ramallah, Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kwa minajili ya
kushiriki kwenye sherehe za kuapishwa.
Wakati huohuo, kiongozi mwingine
wa kisiasa wa Israel amesema kuwa, utawala huo hautafanya tena
mazungumzo na serikali mpya ya Palestima, kwa vile serikali hiyo
inaishirikisha Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina 'Hamas'.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, Mahmoud Abbas Rais wa Mamlaka ya Ndani ya
Palestina amepanga kutangaza baraza la mawaziri hapo kesho, licha ya
kukabiliwa na vitisho vya utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani.
Imepangwa kuwa, Rami Hamdallah atakuwa Waziri Mkuu mpya wa serikali ya
umoja wa kitaifa ya Palestina.
No comments:
Post a Comment