Muhammad Raad, Mkuu wa Mrengo wa Muqawama katika bunge la Lebanon
unaojulikana kwa jina la al Wafaa amesisitiza kuwa, rais ajaye wa nchi
hiyo hatakiwi kuwa kibaraka wa madola ya kigeni. Raad ameongeza kuwa,
rais ajaye anatakiwa azingatie umoja wa kitaifa, awe na uchungu na nchi
yake na pia asiamiliane na maadui kwa lengo la kuidhuru nchi. Ameashiria
kuwa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah haiuungi mkono upande wowote
katika kadhia ya uteuzi wa rais na badala yake anayataka makundi yote ya
kisiasa kuweka kando tofauti zao na kumchagua rais kwa maslahi ya
taifa.
Mkuu huyo wa mrengo wa al Wafaa katika bunge la Lebanon amefafanua
kuwa hii leo taifa la Lebanon limechagua njia ya muqawama na mapambano,
kwani linajua kuwa ni muqawama ndio utakaoiwezesha Lebanon kupata
heshima, kujitosheleza, na kuwa na uhuru wa kweli. Amesema, katika
kulinda uhuru, haki ya kujitawala na kujitegemea, Lebanon haitakubali
uingiliaji wa upande wowote wa kigeni katika masuala yake ya ndani.
Amesema, Bairut itainyoshea nchi yoyote mkono wa urafiki na ushirikiano
chini ya anga ya kuheshimiana. Licha ya wabunge wa Lebanon kufanya vikao
vitano kwa ajili ya kumchagua rais mpya atakayechukua nafasi ya Rais
Michel Suleiman aliyemaliza muda wake tarehe 24 mwezi uliopita wa Mei,
lakini hadi hivi sasa hawajafikia makubaliano.
No comments:
Post a Comment