Wabunge wa Yemen wametaka serikali
ya nchi hiyo ijiuzulu wakisema kuwa imeshindwa kutatua matatizo muhimu
yanayolalamikiwa na wananchi. Yahya Ali al-Raee Spika wa Bunge la Yemen
amesema wazi mbele ya Waziri Mkuu Mohammed Salem Basondowa kuwa
serikali inapaswa kujiuzulu, na kuituhumu kuwa ni kama taasisi iliyojaa
maafisa fisadi. Waziri Mkuu huyo wa Yemen pia amekosolewa vikali na
baadhi ya wabunge kuwa si muaminifu na kwamba ameshindwa kutimiza wajibu
wake.
Hata hivyo Waziri Mkuu wa Yemen
ametupilia mbali madai ya kuhusika katika ufisadi na kuwapa changamoto
wanaomtuhumu wathibitishe tuhuma hizo. Serikali ya maridhiano ya Yemen
iliundwa mwaka 2011 nchini Saudi Arabia baada ya kiongozi wa wakati huo
Ali Abdallah Saleh kulazimika kukabidhi madaraka kwa makamu wake
kutokana na mashinikizo ya wananchi.
No comments:
Post a Comment