Katika hali ambayo utawala wa kifalme wa Bahrain hadi sasa umeshavunja
misikiti 38 nchini humo kwa visingizio tofauti, Mfalme wa Bahrain
amemzawadia Papa Francis wa Kanisa Katoliki, ramani ya kanisa kubwa
linalotarajiwa kujengwa nchini humo. Taarifa zinasema kuwa, Hamad bin
Isa Aal Khalifa, Mfalme wa ukoo wa Aal Khalifa wa Bahrain aliitembelea
Vatican na kukutana na Papa Francis, Kiongozi wa Kanisa Katoliki
Duaniani na kujadiliana naye masuala mbalimbali kama vile amani katika
Mashariki ya Kati, kuishi pamoja kwa usalama na amani wafuasi wa dini
tofauti na kukabiliana na makundi yenye misimamo ya kufurutu mipaka
katika dini.
Kanisa hilo linalotarajiwa kujengwa nchini Bahrain litakuwa
kubwa zaidi kuwahi kujengwa katika nchi za Kiarabu. Wapinzani wa
Bahrain wanasema kuwa, safari ya Mfalme wa Baharin huko Vatican ni hatua
ya kimaonesho yenye lengo la kusafisha taswira ya utawala huo wa
kidhulma ambao kwa miaka kadhaa unawakandamiza raia wanaoandamana kwa
amani, hasa Waislamu wa Kishia wa nchi hiyo. Tangu kuanza harakati za
mapinduzi za wananchi wa Bahrain mwaka 2012 hadi sasa, zaidi ya watu 150
wameshapoteza maisha yao kutokana na ukandamizaji unaofanywa na utawala
wa ukoo wa kifalme wa Bahrain huku mamia wakitiwa mbaroni kwa sababu tu
ya kuandamana na kudai haki zao za kimsingi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment