Msafara wa misaada ya kibinadamu umewasili katika Ukanda wa Gaza
unaozingirwa na Israel, kama sehemu ya jitihada za kuvunjwa mzingiro huo
uliowekwa na Tel Aviv dhidi ya eneo hilo la Palestina. Msafara huo
unaoitwa 'The Miles of Smile 27' umewasili Ukanda wa Gaza kupitia kivuko
cha Misri cha Rafah, huku ukiwa umebeba vifaa vya tiba na misaada ya
kibinadamu. Rashad al Baz mwandamizi wa msafara huo amesema,
wanaandamana na wanaharakati kutoka Algeria na Jordan na kwamba
wamekwenda huko kutokana na furaha ya kufikiwa makubaliano ya umoja wa
kitaifa ya Palestina.
Msafara huo una wanaharakati 25 na watabakia
katika Ukanda wa Gaza kwa siku 3 ambapo watakutana na maafisa wa eneo
hilo na kutembelea maeneo tofauti.
Utawala wa Kizayuni wa Israel unazingira Ukanda wa Gaza tangu Juni
2007, hatua ambayo imepelekea Wapalestina wa eneo hilo kukabiliwa na
matatizo makubwa na kuishi katika mazingira magumu.
No comments:
Post a Comment