Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imewataka raia wote wa Jamhuri ya Kongo
Brazzaville watakaoingia nchini humo, wawe na viza na hati ya
kusafiria. Richard Muyej Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo amesema kuwa, hatua hiyo imechukuliwa ili
kukabiliana na hatua zisizo za kibinadamu zilizoonyeshwa hivi karibuni
na vikosi vya usalama vya Kongo Brazzaville za kuwafukuza raia wa Kongo
Kinshasa nchini humo. Imeelezwa kuwa, uhusiano wa pande hizo mbili
umeingia dosari baada ya serikali ya Kongo Brazzaville kuwafukuza raia
wa Kikongo walioko nchini humo.
Shirika la Kimataifa la Wahajiri
limetangaza kuwa, tokea kuanza operesheni ya kufukuzwa raia wa Kikongo
kutoka nchini Kongo Brazzaville mwezi uliopita, zaidi ya Wakongo elfu 80
wamesharudishwa makwao. Inafaa kuashiria hapa kuwa, mwanzoni mwa mwezi
uliopita, Polisi ya Kongo Brazzaville iliwafukuza wahajiri wa Kikongo
wasiokuwa na vibali vya kuishi nchini humo kwa kisingizio cha
kukabiliana na ongezeko la vitendo vya uhalifu na jinai. Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo ina jumla ya watu milioni 76 huku Jamhuri ya Kongo
Brazzaville ikiwa na jumla ya watu milioni 4 tu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment