Rais Mohamed Ould Abdel Aziz wa Mauritania na ambaye pia ni Mwenyekiti
wa hivi sasa wa Umoja wa Afrika amefanikiwa kuzipatanisha pande hasimu
nchini Mali. Makubaliano hayo yalifikiwa jana ambapo pande hizo
zimekubaliana kuweka chini silaha na kufuata mwenendo wa amani nchini
Mali. Rais Mohamed Ould Abdel Aziz wa Mauritania amesema kuwa,
makubaliano hayo yamefikiwa baada ya mazungumzo kati ya maafisa wa AU na
wawakilishi wa serikali ya Mali na wale waasi wa kaskazini mwa nchi
hiyo. Kwa mujibu wa makubaliano hayo pande mbili zimeahidi kukomesha
mapigano na kujiepusha kuendesha harakati zao katika nchi nyingine za
jirani.
Tangu siku ya Jumamosi iliyopita, mji wa Kidal, umekuwa
ukishuhudia mapigano ya hapa na pale kati ya pande mbili baada ya waasi
wa Tuareg kuudhibiti mji huo. Kwa mujibu wa ripoti rasmi, karibu askari
20 wa serikali wameuawa huku wengine 30 wakijeruhiwa. Weledi wa mambo
wanaitaja Ufaransa kuwa inahusika na mapigano hayo, ambayo ni njia moja
wapo ya kuendelea kubakisha askari wake ndani ya ardhi ya nchi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment