Wizara ya Afya nchini Guinea, imetangaza kuwa, watu 101 wamepoteza
maisha yao kutokana na maambukizi ya ugonjwa wa Ebola. Kwa mujibu wa
wizara hiyo, takwimu hizo ni za kuanzia mwezi Januari mwaka huu hadi
sasa. Aidha wizara hiyo imesema, watu wengine wanane wamekumbwa na
ugonjwa huo hivi karibuni katika eneo la mpaka kati ya Guinea na Liberia
katika mji wa Telimele wamagharibi mwa nchi hiyo. Asilimia 90 ya
waathirika wa virusi vya ugonjwa wa Ebola, hufariki dunia suala
lililopelekea ugonjwa huo kutajwa kuwa wa hatari zaidi.
Mwezi Machi
mwaka huu, virusi vya Ebola viliripotiwa kushuhudiwa katika nchi za
Liberia, Sierra Leone na Mali. Baadhi ya nchi jirani na mataifa hayo
zilichukua hatua kali za kuzuia maambukizi ya virusi hivyo ikiwa ni
pamoja na kufunga mipaka na hata kuzuia safari za ndege kutoka nchi
hizo. Hata hivyo juhudi kubwa zilizochukuliwa na nchi hizo kwa
kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO), zinatajwa kuwa ndiyo
sababu ya kupungua maambukizi na ongezeko la kuenea virusi vya ugonjwa
huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment