Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mara
nyingine amesisitiza ulazima wa kushirikiana na kuunganisha nguvu
kikamilifu katika kuangamiza silaha za mauaji ya kimbari ili kuimarisha
amani na usalama duniani. Dakta Rouhani amesema hayo alipohutubia
Mkutano wa CICA huko Shanghai China na kuongeza kuwa njia pekee ya
kuondoa hatari ya silaha hizo ni kuziangamiza kikamilifu.
Rais wa Iran pia amezitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa
kuimarisha nafasi ya nchi za Asia ili ziwe na taathira katika
kuhakikisha kuwa dunia haina silaha za nyuklia.
Raouhani aidha
amekumbusha kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutokana na sera zake za
ulinzi na misingi ya kidini inapinga silaha za nyuklia lakini inaunga
mkono haki ya nchi zote ya kutumia teknolojia ya atomiki kwa matumizi ya
amani.
No comments:
Post a Comment