Mabadiliko katika hewa ya mjini nchini Uingereza yameanza kutoa
mazingira mazuri kwa Mbbu kuishi, ikiwemo wale wenye uwezo wa kuambukiza
ugonjwa wa Malaria na virusi vijulikanavyo kama 'West Nile virus'.
Utafiti unasema kuwa mazingira ya joto pamoja na vidimbwi vya maji katika nyumba za watu, yanawaleta Mbu karibu na watu.
Mbu wanaopatikana nchini Uingereza hawana uwezo
wa kuambukiza maradhi yoyote, lakini wanasayansi hao wanasema kuwa jambo
la wadudu hao kuzaana katika maeneo ya mjini linaongeza uwezo wa
magonjwa kulipuka.
Wanasayansi hao hata hivyo wanakusanya data
zaidi kuona ikiwa wengi wa wadudu pamoja na aina ya wadudu wenyewe
inaweza kuchangia kwa vyovyote mlipuko wa maradhi au la, hasa katika
maeneo ya mjini.
Kadhalika wanasayansi hao wanasema kuwa kutokana na ongezeko la
viwango vya joto katika maeneo ya mjini,Mbu katika baadhi ya maeneo kama
vile Kusini mwa Ulaya wameweza kusababisha magonjwa.
Pia wanasisitiza kwamba Magonjwa yamelipuka katika baadhi ya mataifa ya Ulaya kutokana na mabadiliko ya tabia ya Mbu.
Zaidi ya aina 30 ya Mmbu wamepatikana nchini Uingereza
"katika maeneo ya vijijini kuna Mmbu wengi zaidi
kwa sababu ya mazingira tofauti tofauti, wengine wanapenda kuishi
katika nyasi , wengine katika vidimbwi, na wengine katika mashimo,''
alisema mmoja wa wataalamu.
"lakini ukienda katika maeneo ya mijini , hakuna Mmbu wengi sana , labda utapa aina mbili au tatu ya Mmbu.
Daktari mmoja kwa jina Callaghan, alisema kuwa
kulikuwa na visa vingi vya ugonjwa wa Malaria kila mwaka nchini
Uingereza , wengi wanaokuwa wanarejea kutoka sehemu mbali mbali za dunia
ambako ugonjwa Malaria unapatikana.
No comments:
Post a Comment