Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Jumuiya ya Ushirikiano
wa Kiislamu OIC amezitaka nchi za Kiislamu kukabiliana na makundi ya
kitakfiri kama lile la Boko Haram la nchini Nigeria. Hamid Reza Dehqani
ameongeza kuwa nchi za Kiislamu na OIC zinapasa kujiweka mbali na
makundi yanayojinasibisha na Uislamu lakini badala yake yamekuwa
yakitekeleza mashambulio ya kigaidi dhidi ya watu wasio na hatia.
Dehqani ameongeza kuwa, wengi kati ya wanachama wa kundi la Boko Haram
si Waislamu, bali wamo Wakristo na wengine wapagani, ingawa Waislamu ni
wachache kwenye kundi hilo. Dehqani amesema kuwa, ripoti zisizo rasmi
zinaonyesha kuwa, asilimia 90 ya wanachama wa kundi la Boko Haram si
Waislamu. Kundi la Boko Haram lilianzishwa mwaka 2002 na raia wa Nigeria
aitwaye Muhammad Yussuf aliyesoma nchini Saudi Arabia. Mwezi uliopita,
kundi hilo liliwateka nyara wanafunzi wasichana wanaokaribia 300 katika
jimbo la Borno, na hadi sasa bado halijawaachilia huru. Inafaa kuashiria
hapa kuwa, neno Boko Haram lina maana ya kwamba 'Elimu ya Kimagharibi
ni haramu', na lengo kuu la kundi hilo ni kuiangusha serikali ya
Nigeria. Kundi hilo limetekeleza mashambulio kadhaa ikiwemo kwenye
misikiti, mashule, mahospitali, ofisi na majengo ya serikali hususan
katika eneo la Kaskazini mwa Nigeria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment