Russia imeitaka serikali ya mpito ya Kiev kuondoa haraka vikosi
vyake katika eneo la mashariki mwa Ukraine, huku ikiamuru kusitishwa
maneva ya kijeshi yanayofanywa na wanajeshi wa Russia katika eneo
linalopakana na Ukraine. Taarifa iliyotolewa leo na ikulu ya Kremlin
imeeleza kuwa, Rais Vladmiri Puttin wa Russia imetaka kuhitimishwa mara
moja kile alichokiita kuwa ni maamuzi ya operesheni za adhabu dhidi ya
wanaharakati wanaoungwa mkono na Moscow kwenye eneo la mashariki la
Ukraine.
Hatua hiyo inaonekana kuwa ni jitihada zinazofanywa na Russia ili
kupunguza mgogoro na nchi za Magharibi. Hata hivyo wanaharakati
wanaoungwa mkono na Russia ambao wanadhibiti majengo ya serikali
mashariki mwa Ukraine na kupigana na vikosi vya serikali ya Kiev wameapa
kukwamisha uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Jumapili, hasa katika
maeneo yaliyotangaza kujitawala ya Donetsk na Luhansk.
No comments:
Post a Comment