Kamanda wa ngazi za juu katika jeshi la Iran amesema taifa hili
halitaruhusu Marekani kukanyaga mstari mwekundu katika mazungumzo ya
nyuklia yanayoendelea kati ya Tehran na kundi la 5+1. Brigedia Jenerali
Masoud Jazayeri amesema mafanikio ya kijeshi na kiulinzi ya Iran ni
mstari mwekundu na kwamba Marekani isijaribu kuwashinikiza
wanadiplomasia wa Tehran wakubali kulegeza kamba katika sekta hiyo.
Afisa huyo mwandamizi wa jeshi la Iran amewataka wanadiplomasia wa
Tehran kuwa macho dhidi ya njama hizo za Marekani na waitifaki wake
kwenye kundi la 5+1.
Katika miezi ya hivi karibuni Marekani imekuwa ikisema kuwa,
makubaliano ya mwisho ya Iran na kundi la 5+1 ambayo yatapelekea
kuondolewa vikwazo vyote dhidi ya taifa hili sharti yajumuishe mambo
mengine yasiyohusiana na kadhia ya nyuklia. Miongoni mwa mambo hayo ni
pamoja na suala la haki za binadamu, wafungwa wa kisiasa, na uwezo wa
kijeshi wa Iran. Washington inataka Tehran ipunguze kasi katika jitihada
zake za kujiimarisha kijeshi na kiulinzi. Iran imesisitiza kuwa
mazungumzo yanayoendelea ni ya nyuklia tu na wala hakuna suala lingine
likatalojadiliwa nje ya kadhia ya nyuklia.
No comments:
Post a Comment