Msemaji wa Rais Vladmir Putin wa Russia amesema kuwa Moscow haitobadili misimamo yake kuhusu Syria na itaendelea kuunga mkono mazungumzo kama njia ya kutatua mgogoro wa kisiasa unaoikabili nchi hiyo ya Mashariki ya Kati. Dmitry Peskov amekosoa hatua ya nchi za Magharibi ya kuwafukuza mabalozi wa Syria katika nchi zao na kusema hatua hiyo itachochea zaidi mgogoro uliopo badala ya kutuliza hali ya Mambo. Msemaji wa Rais Putin amekiri kwamba Marekani na Umoja wa Ulaya zimekuwa zikiishinikiza Moscow kubadilisha misimamo yake kuhusu kadhia ya Syria lakini akasisitiza kuwa siasa za Russia sio bendera ambayo kawaida yake hufuata upepo bali ni siasa zilizojengeka juu ya msingi wa uadilifu na uwazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment