Afisa wa harakati ya Hizbullah ya
Lebanon anayeshughulikia masuala ya kigeni ameutaka Umoja wa Mataifa
uchukue hatua za kukabiliana na chokochoko na mashambulio ya mara kwa
mara ya Israel dhidi ya nchi hiyo. Amar Musawi amesema hayo katika
mazungumzo yake na Derrick Plambly mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa nchini Lebanon na kusema kuwa, mashambulio na ukiukaji wa mara
kwa mara wa mipaka ya ardhi ya Lebanon unaofanywa na Israel umekithiri
na kwamba Umoja wa Mataifa unapaswa kuchukua hatua madhubuti na za
kivitendo kuzuia suala hilo.
Afisa huyo wa harakati ya Hizbullah ya
Lebanon pia ameutaka Umoja wa Mataifa kuzingatia madhara ya mgogoro wa
Syria na hasa kadhia ya wakimbizi wa nchi hiyo walioko Lebanon na jamii
ya kimataifa kuisaidia serikali ya Beirut katika suala hilo.
No comments:
Post a Comment