Shirika la kutetea
haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) limeituhumu serikali ya
Somalia kuwa inatumia vibaya mahakama za kijeshi kuwahukumu bila
uadilifu mamia ya wafungwa huku ikiwanyima haki za kuwa na mawakili wa
kuwatetea.
Shirika hilo limesema
kuwa mamia ya raia wa Somalia wameshitakiwa katika mahakama za kijeshi
na kuhukumiwa bila kuzingatiwa sheria na viwango vya kimataifa. Shirika
hilo la kutetea haki za binadamu pia limesema, raia wengi wamejikuta
matatani baada ya kukamatwa katika msako wa kitaifa unaofanywa na
mashirika ya kijasusi ya Somalia na wengi huwekwa vizuizini kwa muda
mrefu bila kufunguliwa mashtaka.
Human Rights Watch imetoa ripoti
iliyoashiria zaidi ya kesi 24 zilizosikilizwa na kuamuliwa kwa muda wa
chini ya siku 4 na kusema kuwa serikali ya Somalia inapaswa kufanya
mabadiliko na kuhamishia kesi za raia katika mahakama za kawaida.
No comments:
Post a Comment