Omar Nazrin Ntezimbere, balozi wa
Burundi hapa nchini amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepiga
hatua kubwa katika uwanja wa elimu na teknolojia na kusisitiza kwamba
nchi zinazoendelea zinapaswa kustafidi na uwezo wa kielimu na
kiteknolojia wa Iran. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kutembelea kituo cha utafiti wa nyuklia katika mkoa wa Alborz, Balozi
Ntezimbere amesema kuwa, Iran licha ya kupiga hatua kubwa kielimu ni
nchi muhimu ulimwenguni kutokana na kuwa na ustaarabu na utamaduni
mkongwe.
Balozi wa Burundi hapa mjini Tehran ameongeza kuwa, nchi ambazo
zinataka kupiga hatua kimaendeleo zinaweza kushirikiana na Iran katika
nyanja mbalimbali zikiwemo za elimu na teknolojia. Inafaa kuashiria hapa
kuwa, viongozi wa ngazi za juu wa Iran mara kwa mara wamekuwa
wakisisitiza juu ya kulipa kipaumbele bara la Afrika katika sera zao za
kigeni.
Katika upande mwingine Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA
wamekubaliana juu ya hatua mpya tano zitakazochukuliwa ili kuimarisha
zaidi mashirikiano ya pande mbili.
No comments:
Post a Comment