Idadi ya watu waliouawa katika mripuko uliotokea kwenye makao
makuu ya polisi katika mji wa Mansoura huko Misri imeongezeka na kufikia
14. Bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari liliripuka mapema leo
kwenye makao makuu ya polisi ya mji wa Mansoura ulioko umbali wa
kilomita 110 kaskazini mwa Cairo katika wilaya ya Dakahlyia. Jengo zima
limeporomoka na magari kadhaa yaliyokuwa nje ya makao makuu ya polisi
yameharibika kutokana na mripuko huo mkubwa wa bomu uliotokea leo.
Watu 14 wamepoteza maisha katika mripuko huo huku wengine zaidi ya
100 wakijeruhiwa. Sami al Mihi Mkuu wa polisi wa wilaya ya Dakahlyia ni
miongoni mwa watu waliojeruhiwa katika mripuko huo wa bomu huku washauri
wake wawili wakiuawa.
No comments:
Post a Comment