Watu kadhaa wameuawa na wengine kujeruhiwa, baada ya waasi wa Uganda
kushambulia eneo la mpakani mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na
Uganda na kuwalazimisha maelfu ya Wakongo kukimbilia Uganda.
Msemaji wa Jeshi la Uganda Luteni Kanali Paddy Ankunda amesema leo
kuwa, shambulio hilo la waasi wa Allied Democratic Forces (ADF)
limefanyika katika eneo la Kamango, mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo jirani na mpaka wa nchi hiyo na Uganda.
Imeelezwa
kuwa, waasi hao wa ADF bado wanaudhibiti mji huo tokea jana, ingawa
majeshi ya Kongo yanajaribu kuukomboa mji huo.
Wakati huohuo, Karen Ringuette Msemaji wa Shirika la Wakimbizi la
Umoja wa Mataifa UNHCR nchini Uganda amesema kuwa, kwa akali watu elfu
18 wamekimbilia nchini Uganda baada ya kutokea mapigano hayo.
Hadi sasa hakuna takwimu zozote rasmi za watu waliouawa na kujeruhiwa kwenye mapigano hayo.
No comments:
Post a Comment