Serikali ya Tanzania imekanusha madai yaliyotolewa na baadhi ya vyombo
vya habari kwamba viongozi wa Zanzibar walitengwa wakati wa ziara ya
Rais Barack Obama wa Marekani nchini humo. Serikali imesema viongozi
wote wa Tanzania Bara na Zanzibar walishirikishwa na kwamba Rais Ali
Mohammed Shein aliwakilisha watu wa Zanzibar kwenye shughuli hizo.
Serikali imeongeza kwamba Rais Shein alikuwa miongoni mwa viongozi
wachache waliopata fursa ya kumpokea Obama uwanja wa ndege.
Vyombo vya
habari vilikuwa vimeripoti kwamba viongozi wa Zanzibar walizuia
kushiriki kwenye shughuli mbalimbali wakati Rais Obama alipokuwa
Tanzania siku za Jumatatu na Jumanne. Wakati huo huo serikali ya
Tanzania imesema ziara ya Obama ilikuwa na mafanikio makubwa na kwamba
imeiletea heshima nchi hiyo sio tu barani Afrika bali duniani kote kwa
ujumla.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment