Habari kutoka Pakistan zinasema kuwa watu 17 wameuawa katika eneo la
mpakani la Waziristan baada ya ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani
kuwashambulia kwa makombora usiku wa kuamkia leo. Ingawa jeshi la
Marekani limesema kwamba waliouawa ni wanamgambo wa Taliban, lakini
wananchi katika eneo hilo wanasema raia wa kawaida wakiwemo wanawake na
watoto ndio waliouawa. Waziri Mkuu wa Pakistan, Nawaz Sharif amesema
uchunguzi utafanywa na ikibainika kwamba Marekani imewaua raia wasio na
hatia kwenye hujuma hiyo Islamabad itaitaka Washington kuwalipa fidia
waathirika.
Hii ni mara ya kwanza kwa Marekani kutekeleza hujuma ya aina
hiyo katika eneo hilo la kikabila la Waziristan tangu Nawaz Sharif
ashike hatamu za uongozi nchini Pakistan mwezi uliopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment