Serikali ya Sudan imesisitiza kuwa itaendelea kuheshimu makubaliano ya
ushirikiano kati yake na Sudan Kusini. Hayo yamesemwa na Waziri wa
Mafuta wa Sudan, Awad Ahmad al Jaz na kuongeza kuwa, Khartoum inalipa
umuhimu mkubwa suala la kudumishwa usalama na amani kati ya nchi hizo
mbili na kutekelezwa makubaliano yaliyofikiwa baina yao. Katika
mazungumzo yake na na balozi wa Umoja wa Ulaya mjini Khartoum, Bwana al
Jaz amesema kuwa, Sudan haijawahi kuwa na chaguo jingine ghairi ya
kuimarisha usalama katika mipaka ya pamoja na Sudan Kusini na kwamba,
hilo ni kwa manufaa ya nchi mbili katika ramani ya kutekeleza
makubaliano ya pamoja.
Ameongeza kuwa, pamoja na Sudan Kusini
kuvishambulia visima vya mafuta ambavyo ni mali ya Sudan huko katika
eneo la Heglig mwezi Aprili mwaka jana, lakini serikali ya Khartoum
ilikubali kusaini makubaliano ya ushirikiano na serikali ya Juba huku
ikiendelea kusafirisha mafuta ya Sudan Kusini kupitia mabomba yake ndani
ya ardhi ya Sudan. Kwa upande wake, balozi huyo wa Umoja wa Ulaya
nchini Sudan alisisitiza kuwa, ushirikiano na mawasiliano baina ya
Khartoum na Umoja wa Afrika kwa ajili ya kumaliza tofauti zilizopo kati
ya nchi mbili, ni suala la lazima.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment