Zaidi ya mashirika 19 ya kijamii nchini Marekani yamewasilisha kesi
kortini yakiishtaki serikali ya nchi hiyo kwa kufanya ujasusi usio
halali dhidi ya mabilioni ya watu kote duniani. Mashirika hayo yameitaka
mahakama kuishurutisha serikali isimamishe mara moja ujasusi huo.
Mawakili wa mashirika hayo ya kijamii nchini Marekani wamesema hatua ya
serikali ya kudukua baruapepe za watu pamoja na akaunti zao kwenye
mitandao ya kijamii,
kusikiliza mazungumzo ya simu kwa siri na kuweka
vinasasauti katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kunasa
mazungumzo ya wanadiplomasia ni kinyume na katiba ya Marekani na
vilevile sheria za kimataifa. Majuma kadhaa yaliyopita, afisa wa zamani
wa shirika la kijasusi la Marekani CIA Bw. Edward Snowden alifichua kwa
mara ya kwanza mpango huo wa vyombo vya kijasusi vya Washington wa
kuwafanyia ujasusi watu kote duniani. Ufichuzi huo umeiweka pabaya
Marekani na kwa sasa Washington inamtafuta kwa udi na uvumba Bw. Snowden
ili kumfungulia mashtaka ya kile inachosema ni kuhatarisha usalama wa
taifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment