Utafiti uliofanywa na Umoja wa Mataifa kupitia kitendo chake cha
Uchumi na Jamii umeonyesha kuwepo haja ya kuanzisha mikakati mipya ili
kukabiliana na changamoto ya watu wengi kuhamia mijini kunakochangiwa na
mambo mbalimbali ikiwemo mahitaji ya nishati ya umeme, maji, huduma za
umma na elimu.
Kwa mujibu wa utafiti huo, kiasi cha watu bilioni 6.25 watakuwa
wanaishi katika maeneo ya mijini hadi kufikia mwaka 2050 na nusu yao
wanaelezwa kuwa watakuwa wakiishi kwenye maeneo ya ovyo ovyo wakikosa
huduma muhimu kama maji safi na salama, miundombinu bora, umeme na
kukosa huduma za afya na elimu.
Kama hiyo haitoshi utafiti huo unatoa zingatio kwenye eneo la chakula
ukitaka kuwepo mabadiliko makubwa kwenye ulaji wa chakula ili
kukaribisha mlingano wa ulaji chakula hatua ambayo itasaidia kuepuka
kile kinachoelezwa kundi kubwa la chakula kutupwa majalalani.
Shamshad Akhtar, msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusiana na maendeleo ya
uchumi anasemakatika hali ya sasa agenda ya kubadilisha mwelekeo ili
kuwaokoa watu maskini wanaokabiliwa na tatizo la njaa ifikapo mwaka 2015
inaweza isitimie katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara.
No comments:
Post a Comment