Umoja wa Afrika AU umeitaka Sudan kuchukua hatua za lazima za kuwatia
mbaroni wale wote waliofanya mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa kulinda
amani wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika (UNAMID) huko Darfur
magharibi mwa Sudan. Bi. Nkosazana Dlamini Zuma, Mkuu wa Kamisheni ya
Umoja wa Afrika leo ametoa taarifa akilaani shambulizi la kuvizia
lililofanywa na watu wenye silaha dhidi ya doria ya askari wa UNAMID
huko Darfur magharibi mwa Sudan.
Bi Nkosazana ametaka kutiwa mbaroni na
kuhukumiwa watenda jinai hiyo. Taarifa ya AU imesisitiza kuwa hakuna
kitu chochote kinachohalalisha kuuliwa watu wanaojitolea kurejesha
amani huko Darfur. Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika amesema
shambulio hilo la kuvizia halitawavunja moyo walinda amani wao na
wataendeleza jitihada zao za kurejesha amani ya kudumu huko Darfur. Watu
waliokuwa na silaha wamefanya shambulizi la kuvizia dhidi ya wanajeshi
wa kikosi cha kulinda amani cha UNAMID huko Darfur na kuwauwa wanajeshi
saba wa Tanzania na kuwajeruhi wengine 17.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment