Ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma Misri imesema imepokea malalamiko
ambapo rais aliyetimuliwa madarakani Mohammad Mursi anakabiliwa na
tuhuma za ujasusi, kuchochea mauaji ya waandamanaji na kuharibu uchumi.
Katika taarifa, ofisi ya mwendesha mashtaka imesema inachunguza
malalamiko hayo na kwamba inatayarisha faili la mashtaka dhidi ya Mursi
na viongozi wandamizi wa Harakati ya Ikhwanul Muslimin.
Watuhumiwa hao
wanatazamiwa kusailiwa katika siku zijazo. Mashtaka hayo yanakuja karibu
wiki mbili baada ya jeshi kumuondoa madarakani Mursi kufuatia
maandamano yaliyoambatana na umwagaji damu. Huku hayo yakijiri wafuasi
wa Mursi bado wako kwenye mitaa ya Cairo mji mkuu wa nchi hiyo na
wameapa kuendeleza maandamano hadi atakaporejeshwa madarakani.
Kwingineko Waziri Mkuu wa Muda Misri Hazem el-Beblawi amesema wiki ijayo
atatangaza baraza lake la mawaziri katika fremu ya 'ramani ya njia'
inayoungwa mkono na jeshi ili kurejesha utawala mikononi mwa raia.
No comments:
Post a Comment