Mahakama ya Katiba ya Zimbabwe imekataa ombi la serikali ya nchi
hiyo la kubadilisha tarehe iliyoainishwa kwa ajili ya kufanyika uchaguzi
wa rais na bunge. Serikali ya Harare ilikuwa imeitaka mahakama hiyo
kuakhirisha tarehe ya uchaguzi.
Mei 31 Mahakama ya Katiba ya Zimbabwe mwaka huu ilitoa hukumu na
kutangaza kwamba uchaguzi wa rais na bunge wa nchi hiyo unapaswa
kufanyika kabla ya Julai 31 mwaka huu wa 2013.
Suala hilo linapingwa na
wapinzani wa Rais Robert Mugabe ambapo Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan
Tsvangirai anaona kuwa wanahitajia muda zaidi ili kutekelezwa
marekebisho ya kimsingi nchini kabla ya uchaguzi. Uchaguzi wa Rais na
Bunge jipya la Zimbabwe unatazamia kuhitimisha shughuli za serikali ya
mseto na umoja wa kitaifa.
No comments:
Post a Comment