Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, July 5, 2013

EU kukata mikataba na Marekani baada ya ujasusi

Bunge la Umoja wa Ulaya limesema kuwa litafuta makubaliano iliyofikia  huko nyuma na Marekani ya kuiruhusu kuwa na taarifa za usafiri na fedha za nchi za Ulaya, iwapo Washington haitaoa maelezo kuhusu tuhuma za kuzifanyia ujasusi nchi hizo. Sambamba na kulaani hatua ya Marekani ya kuwafanyia ujasusi maafiwa wa EU, bunge hilo limetahadharisha kuwa litasimamisha Makubaliano ya Ushirikiano wa Taarifa na Marekani (TFTP) na pia makubaliano ya Rekodi za Taarifa ya Wasafiri (PNP) iwapo Washington haitotekeleza takwa hilo la nchi za Ulaya.
Makubaliano hayo yalifikiwa kati ya pande mbili baada ya mashambulizi ya Sepetemba 11.
Juni 9 afisa wa zamani wa CIA, Edward Snowden alisema kwamba, Shirika la Usalama wa Taifa la Marekani (NSA) limekuwa likiwachunguza kwa siri na kuwafanyia ujasusi wanadiplomasia wa EU katika miji ya Washington, New York na Brussels. Jambo hilo limelaaniwa vikali na maafisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Ulaya.

No comments: