Serikali ya Nigeria na kundi la Boko Haram, wamekubaliana kusimamisha
mapigano ya pande mbili. Makubaliano hayo yamekuja kwa mnasaba wa
kuwadia mwezi mtukufu wa Ramadhani. Mkuu wa tume ya kufanya mazungumzo
na Boko Haram, Bwana Tanimu Turaki amewambia waandishi wa habari kuwa,
makubaliano hayo ya usitishaji mapigano kati ya serikali na kundi hilo,
yamefikiwa baada ya mazungumzo ya muda mrefu kati ya pande hizo mbili.
Tume hiyo imeundwa na Rais Goodluck Jonathan wa nchi hiyo, kwa lengo
hilo. Aidha tume hiyo yenye wajumbe 26, inafanya juhudi za kuwapokonya
silaha wanamgambo wa kundi hilo. Turaki ameongeza kuwa, mazungumzo hayo
kati ya serikali na kundi la Boko Haram, yamewashirikisha wanachama 104
wa kundi hilo na yamefanyika katika moja ya magereza ya mjini Lagos. Hii
ni katika hali ambayo gavana wa jimbo la Yobe la kaskazini mwa Nigeria
ameamuru kufungwa shule zote za sekondari katika jimbo hilo hadi mwezi
Septemba baada ya kutokea maafa ya kuuawa watu 42 katika shule moja
jimboni humo. Wanafunzi 41 wa shule hiyo ya sekondari na mwalimu wao
mmoja waliuawa katika shambulizi lililofanywa na watu waliokuwa na
silaha na wanaosadikiwa kuwa ni wanamgambo wa Boko Haram katika mji wa
Mamudo, jimboni humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment