Hatimaye usalama umerejea kwenye jengo la idara ya gadi ya rais nchini
Misri. Hatua hiyo imekuja baada ya kupita siku moja ya umwagaji mkuwa wa
damu, katika mapigano yaliyotokea mbele ya jengo hilo la gadi ya rais
kati ya wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani Muhammad Mursi na jeshi
la nchi hiyo na kusababisha zaidi ya watu 50 kuuawa na mamia ya wengine
kujeruhiwa. Usalama umetanda tangu asubuhi huku idadi ya askari
wakipunguzwa eneo hilo.
Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia
Sergey Lavrov, ametangaza kuwa, nchi yake inaunga mkono hatua ya
kurejeshwa usalama na amani nchini Misri. Lavrov ameyasema hayo hii leo
na kuongeza kuwa, Moscow inaunga mkono juhudi zote za kumaliza machafuko
nchini ya Miri na kufanyika uchaguzi huru na wa haki nchini humo. Tangu
alipopinduliwa Rais Muhammad Mursi wa nchi hiyo, taifa hilo la
kaskazini mwa Afrika limekuwa likishuhudia machafuko huku Umoja wa
Afrika ukiwa tayari umesimamisha kwa muda uanachama wa Misri katika
umoja huo. Mapema leo idara ya habari na mawasiliano ya ikulu ya rais
nchini Tunisia, imekanusha kuhusika kivyovyote na suala la kusimamishwa
uanachama wa Cairo katika Umoja wa Afrika. Itakumbukwa kuwa, Tunisia ni
miongoni mwa nchi zilizopinga mapinduzi ya jeshi la Misri dhidi ya Rais
Mursi na kuitaja kuwa ni ukandamizaji wa demokrasia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment