Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya
Nyuklia IAEA amekula kiapo cha kuchukua wadhifa wa Makamu wa Rais nchini
Misri. Muhammad al Baradei amekula kiapo hicho mbele ya Adly Mansour,
Rais wa serikali ya Mpito ya Misri.
Wakati huo huo harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri na mirengo
mingine ya Kiislamu ya nchi hiyo imetoa wito wa kufanyika maandamano ya
mamilioni ya watu dhidi ya serikali ya Adly Mansour, Rais wa serikali ya
mpito ya nchi hiyo.
Wanaharakati wa Misri wametangaza kuwa maandamano hayo yatafanywa
kesho na wafuasi wa Morsi katika meidani za Rabaa Adawiya, Nahdha, al
Jizah, Ramsis na kwenye daraja la Oktoba Sita.
Hii ni katika hali ambayo wapinzani wa Muhammad Morsi, rais wa Misri
aliyeng'olewa madarakani na jeshi la nchi hiyo nao pia wamejiandaa
kikamilifu kufunga barabara zinazoelekea kwenye meidani hizo khususan
kwenye daraja la Oktoba Sita, meidani ya Lebanon na kitongoji cha Nasr
na njia ya chini kwa chini ya Nasr.
No comments:
Post a Comment