Rais Mohammad Mursi wa Misri ameapa kwamba hatoondoka madarakani na
kwamba yuko tayari kufa kwa ajili ya kutetea demokrasia. Akizungumza
usiku wa jana kupitia radio na televisheni ya taifa, kiongozi huyo
aliwaambia wapinzani wake kuwa, alichaguliwa kihalali na kwamba
ataendelea na majukumu yake hadi kipindi chake kitakapomalizika. Wafuasi
wake pia wameapa kumlinda kiongozi huyo na kwamba wako tayari kufa kwa
ajili yake. Wapinzani kwa upande wao wamesisitiza kuwa maandamano
yataendelea hadi pale Dkt. Mursi atakapojiuzulu.
Weledi wa mambo
wanasema Misri inaelekea kutumbukia katika vita vya ndani hususan baada
ya jeshi kusema huenda likachukua jukumu la kuiongoza nchi iwapo pande
hasimu hazitofikia makubaliano kufikia leo jioni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment