Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn ametia saini mkataba wa
ugawanaji sawa wa maji ya Mto Nile miongoni mwa nchi unakopita mto huo.
Bunge la Ethiopia limempa idhidi Waziri Mkuu kusaini mkataba huo, hatua
inayotarajiwa kuongeza msuguano na Misri ambayo kwa sasa inapinga
mipango ya Addis Ababa ya kujenga bwawa kubwa ili kunufauka na maji ya
mto huo. Mkataba huo unachukua nafasi ya mkataba wa zama za ukoloni
ambapo Misri na Sudan ndizo zilizopewa haki kubwa katika utumiaji wa
maji ya Mto Nile.
Misri inatarajiwa kutuma ujumbe wa ngazi za juu
utakaoongozwa na Waziri Mkuu, Hisham Qandil nchini Ethiopia ili
kuishawishi Addis Ababa asimamishe ujenzi wa bwawa la Renaissance. Rais
Muhammad Mursi ametishia kwamba nchi yake iko tayari hata kutumia nguvu
ili kuzuia Ethiopia kujenga bwawa hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment