Sudan imesema kuwa waasi wa Sudan Kusini walishambulia bomba la
mafuta katika eneo lenye mafuta la Diffra siku ya Jumatano, na
kusababisha mlipuko na moto kwa masaa kadhaa. Al Sawarmi Khalid msemaji
wa jeshi la Sudan ameeleza kuwa, bomba hilo linalosafirisha maafuta hadi
kwenye kiwanda cha Heglig limekarabatiwa na kuanza tena kufanya kazi.
Khalid ameongeza kuwa, waasi wa JEM ndio waliofanya shambulizi hilo
kutokea jimbo la Sudan Kusini na walisaidiwa na jeshi la nchi hiyo.
Sudan Kusini imeanusha madai hayo na msemaji wake Makol Arik amesema,
hawawezi kufanya hivyo wakati ambapo wanahitajia mafuta yao
kusafirishwa na Sudan. Nchi hizo mbili kwa muda mrefu zinatuhumiana
kuwaunga mkono waasi wa upande wa pili na hivi karibuni Sudan ilitangaza
kusimamisha usafirishaji wa mafuta ya Sudan Kusini kwa madai kwamba
Juba inasaidia waasi dhidi yake ya Khartoum.
No comments:
Post a Comment