Katika kile kinachoonekana ni kuendelea propaganda dhidi ya serikali
halali ya Syria, Umoja wa Mataifa umetoa ripoti inayosema hadi sasa
zaidi ya watu 93, 000 wameuawa kwenye machafuko nchini humo. ripoti hiyo
imekwenda mbali na kusema maafa mengi yamesababishwa na serikali ya
Rais Bashar Asad. Huku hayo yakijiri, Marekani imezusha propaganda mpya
na kusema sasa upo ushahidi kamili kwamba, serikali ya Syria ilitumia
silaha za kemikali dhidi ya raia.
Rais Barack Obama wa Marekani
ameidhinisha kupewa silaha magaidi wa Syria wanaopigana na serikali
akisema Asad amekanyaga msitari mwekundu. Taarifa kutoka ikulu ya White
House imesema Marekani itatoa misaada ya moja kwa moja ya kijeshi kwa
makundi ya waasi huko Syria na kwamba misaada hiyo itajumuisha silaha
nzito.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment