Wagombea 21 wa nafasi ya urais nchini Madagascar wamewataka wagombea
watatu wa kinyang'anyiro hicho wajiengue kwenye mbio za urais nchini
humo. Wagombea hao 21 kati ya 41 wametangaza kuwa, hawatashiriki kwenye
vikao vya uchaguzi wa rais hadi pale watakapojiondoa wagombea watatu
ambao ni Lalao Ravalomanana, mke wa Marc Ravalomanana Rais wa zamani wa
nchi hiyo, Andry Rajoelina Rais wa serikali ya mpito, na Didier
Ratsiraka rais wa zamani wa nchi hiyo.
Jean Lahiniriko mmoja kati ya
wagombea wa nafasi ya rais katika uchaguzi ujao nchini humo amesema
kuwa, kushiriki kwenye vikao hivyo ina maana ya kuunga mkono ushiriki wa
wagombea hao. Wagombea hao watatu walipuuza takwa lililotolewa na wakuu
wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ustawi ya Kusini mwa Afrika SADC ya
kuwataka wajiengue kwenye kinyang'anyiro hicho cha urais. Kutokana na
kuibuka mivutano hiyo, uchaguzi wa rais nchini humo uliopangwa
kufanyika Julai 24, sasa utafanyika Agosti 23 mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment