Waandamanai wanaopinga serikali ya Rais Mohammad Morsi wa Misri
wamechoma moto ofisi za chama chake cha Uhuru na Uadilifu ambacho ni
tawi la kisiasa la harakati ya Ikhwanul Muslimin. Shirika la habari la
al-Yaum Sub’h limeripoti kuwa, ofisi hiyo ilivamiwa na kuharibiwa kabla
ya kuteketezwa katika mji wa Ibrahimia kaskazini mashariki mwa nchi.
Habari zaidi zinasema kuwa, maafisa waandamizi wa chama hicho waliokuwa
ofisini wakati wa tukio hilo walilazimika kukimbilia usalama wao katika
msikiti uliokuwa karibu. Mali ya thamani kubwa imeharibiwa kwenye tukio
hilo.
Rais Morsi anakabiliwa na mashinikizo makubwa kutoka kwa wapinzani
ambao wanadai uongozi wake wa mwaka mmoja haujaweza kutatua matatizo
yanayowakabili Wamisri wa kipato cha chini. Wapinzani hao wakingozwa na
shakhsia mashuhuri kama vile Mohammad el-Baradei na Amr Musa wamepanga
kufanya maandamano makubwa Juni 30 ili kushinikiza kujiuzuu rais huyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment