Wananchi wa Misri wamekosoa vikali matamshi ya Rais Muhammad Mursi wa
nchi hiyo kuhusiana na Syria na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya
Hizbullah nchini Lebanon. Duru za habari nchini Misri zinaarifu kuwa,
wananchi wa nchi hiyo wamekosoa matamshi ya hivi karibuni ya rais huyo
kwa kuishambulia Harakati ya Hizbullah na hatua yake ya kukata uhusiano
na serikali ya Damascus. Itakumbukwa kuwa hivi karibuni Rais Muhammad
Mursi alitangaza kuwa nchi yake imekata kabisa uhusiano wa kidiplomasia
na serikali ya Syria na kuzitaka nchi za Magharibi kuanzisha eneo la
marufuku ya kupaa ndege nchini humo.
Maneno hayo ya Rais Mursi
yameakisiwa sana nchini humo hasa kwa kuzingatia kuwa, yanaunga mkono
njama za Marekani dhidi ya taifa na watu wa Syria. Ukosowaji huo
haukufanywa na wananchi wa Misri pekee, bali hata baadhi ya majenerali
wa jeshi la nchi hiyo nao wameyataja maneno ya rais huyo kuwa yasiyofaa.
Kabla ya hapo kwa mara kadhaa jeshi la Misri lilikuwa likipinga uungaji
mkono wa serikali ya Cairo kwa waasi wa Syria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment