Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Monday, June 17, 2013

Machafuko yaendelea kushuhiwa mjini Istanbul, Uturuki

Jana usiku mitaa ya mjini Istambul, Uturuki, ilishuhudia machafuko makubwa kufuatia hotuba ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdoğan ya kupuuza matwaka ya wapinzani. Machafuko yalizuka baada ya polisi wa mji huo kuwaondoa kwa nguvu waandamanaji kutoka katika bustani ya Gezi iliyopo katika medani maarufu ya Taksim mjini hapo na kuzusha tafrani katika eneo hilo. Aidha machafuko yalizuka wakati wapinzani wa serikali walipokuwa wakikusudia kumaliza mkusanyiko wa wafuasi wa chama cha ‘Uadilifu na Maendeleo’ kinachoongozwa na Erdoğan waliokusanyika katika uwanja uliokaribu na Medani ya Taksim mahali alipohutubia waziri mkuu huyo.
Kwa mujibu wa baadhi ya duru za polisi nchini Uturuki, watu 221 walitiwa mbaroni hapo jana mjini Istanbul huku wengine 70 wakitiwa mbaroni mjini Ankara. Waandamanaji pia wamelaani vikali msimamo wa Erdogan wa kuunga mkono magaidi wanaotaka kuiangusha serikali ya wananchi wa Syria. Waturuki sasa wanataka Waziri Mkuu Erdogan ajiuzulu na kuitishwa uchaguzi wa mapema nchini humo.

No comments: