Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, June 18, 2013

Wajumbe maalumu wajalidi usalama wa Darfur

Wajumbe maalumu kutoka nchi mbalimbali za za dunia, wamejadili hali ya usalama wa Darfur katika kikao kilichofanyika mjini al Fashir katikati ya jimbo hilo. Jana wajumbe maalumu wa Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na baadhi ya nchi kama vile Marekani, Uchina, Russia, Canada, Japan na kadhalika waliendelea na kikao chao cha tano kilichofanyika katika ofisi za Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika huko Darfur.
Washiriki wa kikao hicho walisisitizia udharura wa kufanyika juhudi za jamii ya kimataifa kwa ajili ya kuimarisha usalama na uthabiti wa jimbo hilo na kuyaingiza makundi ya wabeba silaha katika mwenendo wa mazungumzo ya amani jimboni humo. Katika kikao hicho kilichojadili pia makubaliano ya amani yaliyofikiwa mjini Doha, Qatar, kamanda mkuu wa jimbo hiloat-Tijani as-Sisi, alisisitiza juu ya haja ya kutekelezwa makubaliano hayo ya amani ya Doha, ambayo aliyataja kuwa ni hatua muhimu kuelekea amani na uthabiti katika jimbo hilo. Aidha kamanda huyo ameyakosoa makundi ya waasi yanayofanya shughuli zao katika maeneo kadhaa ya Sudan na kuongeza kuwa, makundi hayo yenye ngome zao nchini Sudan Kusini, yamekuwa yakifanya njama za kuharibu mahusiano kati ya Kharoum na Juba.

No comments: