Ujumbe wa kidiplomasia wa Ethiopia ukiongozwa na Naibu Waziri wa Mambo
ya Nje na mkuu wa kituo cha amani wa nchi hiyo, wamewasili mjini Cairo,
Misri kwa ajili ya kushiriki katika kikao cha siku tatu mjini humo. Hii
ni mara ya kwanza kwa ujumbe wa kidiplomasia wa Ethiopia kufanya safari
nchini Misri tangu serikali ya Addis Ababa ilipotangaza kujenga bwawa la
an-Nahdha na kuibuka mzozo kati ya nchi mbili. Weledi wa kimataifa
wanaamini kuwa, ujenzi wa bwawa hilo katika mto Nile, hauwezi kuathiri
maslahi ya nchi za Sudan na Misri.
Weledi hao wa kimataifa kutoka nchi
za Ethiopia, Sudan, Misri, Ufaransa, Ujerumani, Afrika Kusini na
Uingereza, wameanza kufanya uchunguzi wa athari zinazoweza kutokea
kutokana na kujengwa bwawa hilo. Hivi karibuni Waziri Mkuu wa Ethiopia,
Hailemariam Desalegn alitia saini mkataba wa ugawanaji sawa wa maji ya
Mto Nile miongoni mwa nchi unakopita mto huo. Hii ni katika hali ambayo,
Rais Yoweri Museven wa Uganda ametangaza kuiunga mkono serikali ya
Addis Ababa juu ya kujenga bwawa hilo kwa ajili ya kuzalisha umeme. Kwa
upande wake gazeti la The Wall Street Journal limeripoti kuwa, Ethiopia
na nchi nyingine za Afrika zenye kutumia mto Nile, zinahitaji kujenga
mabwawa kwa ajili ya kujizalishia umeme wao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment