Idara inayofuatilia mapato na utajiri wa raia wa Misri kinyume cha
sheria ambayo ni kitengo katika Wizara ya Sheria ya nchi hiyo,
imeongeza muda wa siku 15 za kuendelea kuwashikilia wana wa dikteta wa
zamani Hosni Mubarak kwa ajili ya kuwafanyia mahojiano zaidi. Habari
kutoka Cairo zinaarifu kuwa Alaa na Jamal wakiwa na ulinzi mkubwa,
walifikishwa katika idara hiyo ya Wizara ya Sheria kwa tuhuma za kutumia
vibaya madaraka ya baba yao wakati akiwa rais wa nchi hiyo na
kujikusanyia utajiri mkubwa, kumiliki hisa nyingi katika benki na
kumiliki mali nyingine nyingi kinyume cha sheria.
Kikao cha mahakama kwa
ajili ya kuchunguza faili la wana hao wa dikteta Mubarak, kinatazamiwa
kufanyika leo Jumatatu. Hii ni katika hali ambayo tangu mwezi Mei mwaka
2011 idara hiyo inayochunguza mapato ya raia wa nchi hiyo,
imekwishawahoji Alaa na Jamal kwa tuhuma hizo huku kukiwa
hakujachukuliwa hatua yoyote dhidi yao. Hivi karibuni pia Mahmud
al-Hafnawi, mwakilishi wa mwendesha mashtaka mkuu nchini Misri aliutaja
utajiri wa Mubarak na familia yake kuwa unafikia karibu dola bilioni
moja na milioni 200.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment