Uvaaji wa hijabu na nguo nyingine zenye kuonyesha nembo ya kidini
umepigwa marufuku kwenye mashule na vyuo vikuu vya kusini mwa Russia.
Gavana wa Jimbo la Astrakhan nchini Russia amesema kuwa, kuanzia mwezi
Septemba mwaka huu ni marufuku kuvaa mavazi yenye kuonyesha nembo ya
kidini kwenye shule na vyuo vikuu vilivyoko katika jimbo hilo. Ameongeza
kuwa, Russia ni nchi ya kisekula, hivyo inapasa kukabiliana na baadhi
ya makundi ya kikabila na kidini yanayotaka kudhihirisha itikadi na
imani zao kwenye taasisi za elimu katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa sensa
iliyofanyika mwaka 2012, asilimia 46 ya wananchi wa jimbo la Astrakhan
ni Wakristo wa Madhehebu ya Orthodox, asilimia 16 ni Waislamu na
iliyosalia ni wafuasi wa dini na madhehebu nyinginezo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Hii ni aibu kwa Taifa la Russia ambalo linaitikadi ya kiislamu kutaka wasivae hijabu vyuoni
Post a Comment