Rais Vladmir Putin wa Russia ametangaza kuwa tayari serikali ya Moscow
kupeleka askari wa kulinda amani katika milima ya Golan, kuchukua nafasi
ya vikosi vya Austria. Serikali ya Austria imetangaza kuvitoa vikosi
vyake katika eneo la milima ya Golan, kwa kuhofia usalama wa askari
wake. Rais Putin amesisitiza kuwa, kuna udharura mkubwa wa kuwepo askari
wa kulinda amani katika eneo hilo kutoka na hali tete iliyoko kati ya
Syria na utawala wa Kizayuni wa Israel. Baada ya kujiri mapigano karibu
na maeneo ya milima ya Golan, mara kadhaa makundi ya kigaidi yamekuwa
yakiwakamata mateka askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa katika
eneo hilo. Vikosi vya Umoja wa Mataifa vilipelekwa katika eneo la milima
ya Golan mwaka 1974 kwa lengo la kuhifadhi usitishaji mapigano kati ya
utawala wa Kizayuni wa Israel na Syria. Kabla ya Austria, Japan na
Ukraine zilishaondoa wanajeshi wake katika eneo la milima ya Golan ya
Syria inayokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Hao Russia mbona wanapenda malumbano; wanaiga sera za Marekani
Post a Comment