Ufaransa ambayo ni moja ya nchi zinazounga mkono makundi ya kigaidi
dhidi ya serikali ya Syria, imetangaza wasiwasi iliyonayo kutokana na
kile ilichosema ni uwezekano wa kurejea kwa magaidi hao barani Ulaya.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Manuel Valls, amefichua kuwa, tangu
tarehe 15 Machi mwaka 2011 baada ya kuanza machafuko nchini Syria,
zaidi ya raia wa nchi za Ulaya wapatao 600 wakiwamo Wafaransa 120
waliwasili nchini Syria na kujiunga na makundi ya kigaidi katika vita
dhidi ya serikali ya Damascus na kwamba, hadi sasa kuna Wafaransa 40
ambao bado wako nchini humo. Manuel ameyasema hayo katika kikao cha
kukabiliana na ugaidi barani Ulaya, kilichohudhuriwa na viongozi wa
Ulaya huko nchini Luxembourg na kusisitiza juu ya udharura wa umoja huo
kupanga mikakati ya kukabiliana na vitisho vya vijana wa nchi hizo
wanaopigana nchini Syria. Amesisitiza kuwa, suala la kusikitisha ni
kwamba, wengi wa vijana hao wamejiunga na makundi ya kigaidi ya Al-Qaida
na Jabhat Nasra.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment