Zaidi ya wanamgambo 7000 wa kundi la Muungano wa
Seleka, waasi wa zamani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, wameamua
kuweka chini silaha zao.
Hayo yamesemwa leo na mmoja wa makamanda wa ngazi za juu wa
kikosi cha Afrika cha kulinda amani nchini humo MISCA. Ameongeza kuwa,
wanamgambo wa Seleka wameanza kupewa hifadhi kwenye kambi na kiasi
kidogo tu ndio wako nje ya kambi.
Kiongozi huyo ambaye hakutaka kutaja
jina lake amesema kuwa, vikosi vya majeshi ya Kiafrika viko nchini humo
kwa shabaha ya kurejesha amani na utulivu Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya
Afrika ya Kati, ambapo zaidi ya watu 600 wameuawa katika kipindi cha
wiki mbili zilizopita.
Nalo Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi
(UNHCR) limetangaza kuwa, karibu watu laki mbili na elfu kumi
wameyakimbia makazi yao baada ya kushadidi machafuko mjini Bangui.
No comments:
Post a Comment