skip to main |
skip to sidebar
Iran yakanusha kupanga mauaji ya wanadiplomasia mbalimbali duniani
Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amekanusha habari iliyochapishwa Jumatatu na gazeti la Washington Post inayoituhumu Tehran kuwa inapanga njama ya kuwaua wanadiplomasia wa Marekani, Saudi Arabia na utawala haramu wa Israel katika nchi kadhaa duniani. Mohammad Khazaee amesema kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa katika mstari wa mbele wa kupinga aina yoyote ya ugaidi duniani. Mwanadiplomasia huyo wa Iran amekumbusha kuwa Taifa na wananchi wa Iran ndio wamekuwa wahanga wa ugaidi kufuatia kuuawa wanasayansi wa nyuklia, maafisa wa ngazi za juu na hata kutekwa nyara wanadiplomasia wao. Gazeti la The Washington Post liliandika kwenye makala yake ya Jumatatu kwamba wanadiplomasia wa Riyadh, Tel Aviv na Washington ni miongoni mwa walengwa wa eti njama hizo za Iran.
No comments:
Post a Comment