Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, watu wasiopungua 93,000
wameuawa nchini Syria katika mapigano ya wanamgambo wanaofadhiliwa na
nchi za kigeni dhidi ya serikali ya Rais Bashar al Assad kwa zaidi ya
miaka miwili sasa. Navi Pillay Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa
Umoja wa Mataifa amesema kuwa, tangu Julai mwaka uliopita watu 5,000
wamekuwa wakiuawa kila mwezi kwenye mapigano hayo.
Pillay ameongeza
kuwa, takwimu hizo ni za kipindi cha kati ya Machi mwaka 2011 hadi
mwishoni mwa Aprili 2013 na kwamba kati ya wahanga hao wa vita nchini
Syria, 6,561 ni vijana wadogo na zaidi ya 1,729 ni watoto walio na umri
chini ya miaka 10.
Katika upande mwingine Marekani imesema kuwa inaongeza msaada wa
kijeshi kwa waasi wa Syria wanaopigana dhidi ya serikali, kwa madai kuwa
Damascus eti imetumia silaha za kemikali kwenye mapigano hayo dhidi ya
waasi.
No comments:
Post a Comment