Kiogozi mmoja nchini Msumbiji amearifu kusimamishwa shughuli za
usafirishaji makaa ya mawe katika eneo la mkoa wa kaskazini magharibi
nchini humo. Hatua hiyo imekuja kufuatia kuongezeka wasi wasi wa hali ya
usalama inayoweza kuikabili sekta ya usafirishaji wa njia ya treni
'Sena' baada ya chama kikuu cha upinzani Renamo kutoa vitisho kuhusiana
na suala hilo. Mkuu wa mkoa wa Tete Rachid Gogo, ameiambia redio ya nchi
hiyo kuwa maafisa wa shirika la Rio Tinto wameamua kusimamisha shughuli
za usafirishaji wa bidhaa hiyo kwa kuhofia hasara inayoweza kuwapata
kutokana na vitisho hivyo.
Ni vyema kuashiria hapa kwamba, Shirika la
Rio Tinto hujishughulisha na uvumbuaji na uchimbaji madini katika nchi
mbalimbali. Hivi karibuni wafuasi wa chama tawala cha Frelimo nchini
Msumbiji walifanya maandamano makubwa ya kitaifa siku ya Jumamosi kwa
lengo la kulaani hujuma za hivi karibuni zinazodaiwa kutekelezwa na
wafuasi wa chama kikuu hicho cha upinzani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment