Mamilioni ya wananchi wa Iran leo wanaelekea katika vituo vya
kupigia kura ili kushiriki katika uchaguzi wa rais hapa nchini. Karibu
Wairani milioni 51 wametimiza masharti ya kupiga kura na leo
wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika duru ya 11 ya
uchaguzi wa rais inayofanyika sambamba na uchaguzi wa duru ya 4 wa
mabaraza ya miji na vijiji nchi nzima.
Kampeni za uchaguzi zilimalizika rasmi jana asubuni ambapo wagombea 6
wa uchaguzi huo walihitimisha kampeni zao kwa kusisitiza ilani zao za
uchaguzi katika mikoa tofauti. Wagombea hao watakaopimana nguvu leo ni
mwakilishi mkuu wa Iran katika mazungumzo ya nyuklia Saeed Jalili,
kamanda wa zamani wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Mohsen
Rezai, mwakilishi wa zamani wa Iran katika mazungumzo ya nyuklia Sheikh
Hassan Rohani, waziri wa zamani wa mawasiliano Mohammad Gharazi, meya wa
Tehran Mohammad Bager Qalibaf na waziri wa zamani wa mambo ya nje Ali
Akbar Velayati.
No comments:
Post a Comment